Mojawapo ya Jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapeleka mahakamani mahabusu na kuwarudisha magerezani.

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini.

Gadi ya askari Wanawake na Wanaume wa Jeshi la Magereza katika Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa.

Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja(kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Magereza Barani Afrika nchini Namibia.

Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja(kushoto) akimpongeza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Namibia katika sherehe za kumuaga kufuatia kustaafu kwake Februari 01, 2014 nchini Namibia.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Emilio Mwai Kibaki(wa pili kushoto) akiangalia kazi za mikono zinazofanywa na Wafungwa katika Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga, Dar es Salaam.

Ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa ni sehemu ya miradi ya Uzalishaji inayoendeshwa na kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini.

Sehemu ya Mashamba makubwa yanayoendeshwa na Jeshi la Magereza: Shughuli za Kilimo cha Mashamba makubwa, madogo na bustani za mboga mboga ni moja ya shughuli za Magereza katika kuwafunza wafungwa namna ya kujitegemea mara wamalizapo vifungo vyao.

Baadhi wa wafungwa katika Kiwanda cha Ushonaji nguo cha Gereza Kuu Ukonga wakiwa kazini: Shughuli za Ushonaji wa nguo ni moja ya eneo ambalo wafungwa hupata huduma za urekebishwaji kwa vitendo.

Monday, May 25, 2015

Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi afungua kikao cha bajeti ya shirika la Magereza kwa mwaka 2015/2016 leo mkoani Morogoro

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(suti nyeusi) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja mara baada ya kuwasili leo Mei 25, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Edema, Mkoani Morogoro kwa ajili ya ufunguzi wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka 2015/2016(wa pili kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(hayupo pichani) kutoa hotuba ya ufunguzi wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka 2015/2016.
Wajumbe wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka 2015/2016 wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi leo Mei 25, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Edema, Mkoani Morogoro.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimkabidhi Begi lenye makabrasha ya Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(wa kwanza kulia) ni  Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka 2015/2016 waliosimama(wa tatu kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa tatu kulia) ni  Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Thursday, April 9, 2015

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Tanzania Bw. John Casmir Minja ashiriki mahafali ya kumaliza mafunzo ya awali ya uaskari magereza nchini Uganda

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania Bwn.John .C.Minja akiwaongoza Wakuu wa Magereza wanachama wa ACSA (Umoja wa Nchi zinazoshughulika na Urekebishaji/Magereza Barani Afrika wakati wakiingia Viwanja vya Kololo Jijini Kampala,Uganda kabla ya kuanza kwa ratiba ya kumaliza Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza Nchini Uganda.Shughuli zilizofanyika leo tarehe 9 April,2015 katika Viwanja Kololo Kampala.Aliyeongozana nae ni Mkuu wa Magereza Nchini Angola.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania Bw. John .C. Minja aliyekaa katikati,amevaa nguo za kijana akiwa amekaa na Wakuu Wengine wa Magereza Wanachama wa ACSA wakimsubiri Mgeni rasmi katika Mahafali hayo Mhe. Yoweri Kaguta Mseveni Rais wa Jamhuri ya Uganda,hata hivyo hakuweza kuja na badala yake aliwakilishwa na Makamu wa Rais Nchini Uganda Mhe. Edward Sekand

Sunday, March 29, 2015

Askari magereza aliyekamatwa na fedha bandia afukuzwa kazi

Jeshi la Magereza nchini limemfukuza kazi askari wake wa Gereza Bariadi, Mkoani Shinyanga (pichani) kwa kosa la kupatikana na fadha za bandia kinyume na Sheria za Nchi.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa jana Machi 28, 2015 na kusainiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja, askari Na. B. 6499 Wdr. Edmund Masaga amefukuzwa kazi kwa fedheha kuanzia Machi 28, 2015 kwa kosa la kulidhalilisha Jeshi mbele ya Umma kinyume na Kanuni 22(xlix) ya Kanuni za Utumishi wa Jeshi la Magereza za Mwaka 1997.

Aidha, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja amekemea vikali vitendo hivyo kwani ni kinyume cha Maadili na Utendaji ndani ya Jeshi la Magereza huku akiwataka askari wote wa Jeshi la Magereza nchini kutenda kazi zao kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.


Imetolewa na; Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM
Machi 29, 2015.

Saturday, March 21, 2015

Kamishna Jenerali wa Magereza avisha vyeo maafisa wa jeshi la Magereza, jijini Dar es Salaam

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza(CGP), John Casmir Minja akimvisha cheo cha Kamishna Msaidizi wa Magereza, Afisa Mwandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jeremiah Katungu katika hafla ya uvishaji vyeo kwa Maafisa waliopandishwa vyeo ngazi mbalimbali(jana) Machi 20, 2015 katika Viwanja ya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja akikagua Gadi Maalum ya Heshima iliyoandaliwa na Maafisa wa Jeshi la Magereza katika hafla ya uvishaji vyeo kwa Maafisa waliopandishwa vyeo ngazi mbalimbali(jana) Machi 20, 2015 katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam.
Bendi ya Jeshi la Magereza ikipita mbele ya Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) kutoa heshima baada ya zoezi la uvishaji vyeo Maafisa 77 wa vyeo mbalimbali kukamilika
Maafisa wa Jeshi la Magereza Nchini pamoja na Wageni Waalikwa wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) katika hafla ya zoezi la uvishaji vyeo kwa Maafisa 77 wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Wanawake vyeo mbalimbali(waliosimama nyuma) baada ya zoezi la uvishaji vyeo hivyo Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam(wa pili kushoto) ni Kamishna Huduma za Urekebishaji, Injinia Dionice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Erasmus Kundy. 

Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.

Thursday, March 19, 2015

Kamishna jenerali wa magereza nchini kuvisha vyeo maafisa waandamizi wa magereza mkoa wa Dar es Salaam

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(pichani) kesho tarehe 20 Machi, 2015 saa 8:00 mchana atawavisha vyeo Maafisa wa Jeshi la Magereza wa ngazi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam waliopandishwa vyeo kwa mujibu wa Sheria.

Kwa Mamlaka aliyopewa kisheria na Tume ya Polisi na Magereza ya Mwaka 1990, Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini atawavisha vyeo hivyo katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.

Tume ya Polisi na Magereza katika Kikao chake Namba 2/2014/2015 kilichofanyika tarehe 16 Machi, 2015 chini ya Mwenyekiti Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Ame Silima(Mb) imewapandisha vyeo Maafisa 292 wa ngazi mbalimbali kuanzia tarehe 16 Machi, 2015.

Maafisa hao waliopandishwa vyeo ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza kuwa Kamishna Msaidizi wa Magereza 11, Mrakibu wa Magereza kuwa Mrakibu Mwandamizi wa Magereza 41, Mrakibu Msaidizi wa Magereza kuwa Mrakibu wa Magereza 83 na Mkaguzi Msaidizi wa Magereza kuwa Mkaguzi wa Magereza 157.

Imetolewa na; Inspekta Lucas Mboje, Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM
19 Machi, 2015.

Tuesday, March 17, 2015

Wafungwa gereza kuu Ukonga, Dar es Salaam mahiri kwa ushonaji wa nguo za aina mbalimbali magereza

Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam wakikata vitambaa vya nguo kabla ya kuanza kushona nguo za Wafungwa Magerezani. Wafungwa hao hujifunza Stadi mbalimbali za ujuzi ambazo huwasaidia kujipatia kipato mara tu wanapomaliza kifungo chao.
Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam wakiendelea na ushonaji wa nguo za aina mbalimbali kama wanavyoonekana katika picha. Jeshi la Magereza nchini linatekeleza ipasavyo jukumu lake la Urekebishaji kwa kuwapatia ujuzi wa fani mbalimbali Wafungwa wanapokuwa wakitumikia vifungo vyao Magerezani.
Mkuu wa Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Ismail Mlawa akiongea na Wanahabari(hawapo pichani).
Aina za nguo mbalimbali ambazo tayari zimeshonwa kwa Ustadi Mkubwa na Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga Dar es Salaam. Gereza Kuu Ukonga Dar es Salaam limejizolea umaarufu mkubwa hapa nchini kwa kutekeleza ipasavyo Programu mbalimbali za Urekebishaji wa Wafungwa kwa Vitendo.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Saturday, March 14, 2015

Mafunzo ya awali ya askari wa magereza kozi na. 27 yaendelea vyema chuo Kiwira, Mbeya

Askari Wanafunzi(Recruits) wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza Kozi Na. 27 wakiendelea na masomo kwa vitendo katika Gwaride la silaha kama wanavyoonekana kikakamavu wakiwa na Walimu wao uwanjani huku silaha zao zikiwa begani.
Askari Wanafunzi wa Mafunzo ya Uaskari Magereza Kozi Na. 27 wakiendelea na somo la Gwaride la Salaam ya Utii wakiwa na silaha kama inavyoonekana katika picha.
Bango Kuu linaloonyesha unapoingia Chuo cha Mafunzo ya Uaskari Magereza kilichopo Kiwira, Mkoani Mbeya.
Askari Wanafunzi wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza wakiendelea na masomo ya Darasani. Katika Mafunzo hayo hujifunza masomo mbalimbali ikiwemo Utawala na Uendeshaji wa Magereza, Sheria zinazoongoza Jeshi la Magereza, Ustawi wa Jamii, Afya, Uraia na Utawala na Uongozi

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).