Wednesday, August 13, 2014

Kamishna Generali wa Magereza Nchini akutana na ujumbe kutoka kwa kampuni ya Equator Automech jijini Dar es Salaam

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akisisitiza jambo katika  mazungumzo na Ujumbe Maalum kutoka Kampuni ya Equator Automech inayojishughulisha na uunganishaji Magari na Matrekta hapa Nchini. Kampuni hiyo ipo katika mazungumzo ya Awali ya kuingia Ubia na Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza katika miradi mbalimbali ya Uzalishaji ikiwemo ya Kilimo. Ujumbe huo umefanya mazungumzo hayo leo Agosti 13, 2014 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Equator Automech, Robert Ndege(wa kwanza kushoto) akielezea namna Kampuni yake itakavyoshrikiana na Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza katika miradi mbalimbali ya Uzalishaji ikiwemo ya Kilimo(katikati) ni Mkurugenzi Mshauri wa Kampuni hiyo, Ahmed Bakari akifuatilia mazungumzo hayo.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia mazungumzo ya namna Kampuni ya Equator Automech itakavyoshrikiana na Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza katika miradi yake ya Kilimo. Mazungumzo hayo yamefanyika leo Agosti 13, 2014 Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga(katikati) ni Mkuu wa Kitengo cha Kilimo na Mifugo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro(wa kwanza kushoto) ni Mthibiti wa Fedha wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Gideon Nkana(wa pili kushoto) ni Mwanasheria wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Issack Kangura(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).