Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil
akitoa hotuba ya Ufungaji wa Mkutano wa Wadau uliohusu upokeaji wa maoni
ya Sera ya Taifa ya Magereza. Mkutano huo wa siku mbili umefanyikia
katika Hoteli ya Livingstone Bagamoyo ambapo wadau wamepitia rasimu hiyo
na kutoa maoni kikamilifu Novemba 05, 2014.
Wadau wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungaji wa Mkutano wa Wadau
uliohusu upokeaji wa maoni ya Sera ya Taifa ya Magereza Novemba 05, 2014
katika Hoteli ya Livingstone Bagamoyo .
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo
mafupi kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil kutoa hotuba ya Ufungaji wa Mkutano wa
Wadau uliohusu upokeaji wa maoni
ya Sera ya Taifa ya Magereza.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati)
akipitia makabrasha wakati wa majadiliano ya rasimu ya Sera ya Taifa ya
Magereza(kulia) ni Mkurugenzi Idara ya Malalamiko Wizara ya Mambo ya
Ndani, Bw. A. Shio(kushoto) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Bw. Mbarak Abdulawaki.
Mchumi kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Deonesia Mjema akichangia maoni
katika rasimu ya Sera ya Taifa ya Magereza kabla ya Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil
kutoa hotuba ya Ufungaji wa Mkutano wa Wadau uliohusu upokeaji wa maoni
ya Sera ya Taifa ya Magereza.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma malewa akitolea
ufafanuzi wa Haki za Wafungwa wanazostahili kupatiwa wawapo Magerezani
wakati wa majadiliano Sera ya Taifa ya Magereza Novemba 05, 2014 katika
Hoteli ya Livingstone Bagamoyo(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la
Magereza).