Thursday, October 15, 2015

Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne shule ya sekondari Bwawani

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil

Na Lucas Mboje, Dar es Salaam;

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(pichani) kesho Oktoba 16, 2015 anatarajia kuwa Mgeni rasmi kwenye sherehe za Mahafali ya kumi na mbili ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Bwawani iliyopo Mkoa wa Pwani.

Kwa mujibu wa Taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyotolewa leo Jijini Dar es Salaam na kusainiwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja inasema jumla ya Wanafunzi 95 wa Shule hiyo wanatarajia kuhitimu elimu yao ya Kidato cha Nne Novemba Mwaka huu.

Taarifa hiyo inasema Mgeni rasmi atafanya mambo yafuatayo ikiwemo kuweka jiwe la msingi jengo la maabara, uzinduzi wa mradi wa maji kwenda kwenye majengo ya Kidato cha tano na sita, kuangalia Maonesho ya Taaluma kwa Wanafunzi Washiriki, kutoa vyeti na zawadi mbalimbali kwa Wanafunzi wahitimu na kutoa hotuba.

Shule ya Sekondari Bwawani inamilikiwa na Jeshi la Magereza, ilianzishwa Mwaka 1978 kwa lengo la kutoa elimu ya Sekondari kwa Watumishi wa Magereza ambapo hivi sasa Shule hiyo inatoa elimu ya Sekondari kwa Vijana wa kike na kiume kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini kuanzia Kidato cha kwanza hadi cha sita.